Image
Image

Wafugaji wavamizi watakiwa kuondoka mkoani MANYARA.

MKUU wa wilaya ya BABATI mkoani MANYARA, CRISPIN MEELA, amewapa wafugaji walioingiza mifugo wilayani humo kinyume cha utaratibu, muda wa siku saba wawe wameondoa mifugo yao lasivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria
MEELA ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea kijiji cha VILIMA VITATU na kupewa taarifa kuwa baadhi ya wafugaji kutoka nje ya wilaya hiyo wamehamia kijijini hapo wakiwa na kundi la mifugo yao bila kufuata taratibu na kufanya uharibifu wa mazingira hususan kwenye mapitio ya wanyamapori (ushoroba)
Taarifa ya kijiji hicho imebainisha kuwa kuna maboma 21 ya wafugaji walioingia kijijini hapo wakitokea maeneo mbalimbali huku baadhi yao wakiwa wamekaribishwa na wafugaji wenzao wenyeji na kuchunga mifugo yao katika eneo ambalo kijiji kimepanga kuwa  hifadhi ya jamii ya wanyamapori.
Akizungumza kwenye mkutano wa kijiji, Mkuu wa wilaya ya BABATI, CRISPIN MEELA, amewaagiza wafugaji hao waondoke wilayani mwake  mara moja.
MEELA amewashauri pia wafugaji kubadilisha mfumo wao wa ufugaji wa kuhamahama na mifugo badala yake wafuge kisasa ili kuongeza tija ya mifugo yao
Viongozi wa kijiji hicho cha vilima vitatu wamemweleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wameunda kamati maalumu  iliyopewa kazi ya kubaini wafugaji walioingia katika kijiji chao kinyemela.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment