Rais wa Afrika Kusini atolewa hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyongo.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameripotiwa kutolewa hospitalini siku ya Jumapili baada ya kufanikiwa kufanyiwa upasuaji na kuondolewa vijiwe vya nyongo.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na msemaji wa ikulu ya rais, Zuma mwenye umri wa miaka 73 alifanyiwa upasuaji usiku wa Jumamosi.
Maelezo zaidi yanaarifu kuwa madaktari walifahamisha kuridhishwa na matokeo ya upasuaji huo, na kusema kwamba Zuma atalazimika kupumzika nyumbani kwa siku kadhaa.
Zuma pia ataendeleza shughuli zake za kazi akiwa nyumbani wakati wa kipindi hicho cha mapumziko.
Zuma aligunduliwa kuwa na vijiwe vya nyongo miezi miwili iliyopita wakati alipofanyiwa ukaguzi wa kiafya.
Mbali na tatizo la nyongo, Zuma pia anaarifiwa kusumbuliwa na maradhi mengine ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari na ugonjwa wa moyo.
0 comments:
Post a Comment