Mkoa wa geita na viunga vyake
umezizima kwa muda wakati mgombea wa kiti cha urais wa chama cha mapinduzi (CCM)Dk.John
Pombe Magufuli alipokuwa akitambulishwa na kuagwa na wapigakura wake wa
jimbo la geita huku wananchi wakimtaja
kama mkombozi wa kulivusha taifa
kuelekea katika haki na usawa kwa watanzania wote.
Akiwa
njiani kutokea mkoani mwanza kuelekea mkoani geita katika eneo la chato
alikozaliwa msafara wa dr magufuli ulijikuta ukisimamishwa njiani mara kwa mara
na umati mkubwa wa wananchi bila ya kujali jinsia na rika waliojitokeza
barabarani kwa lengo la kutaka kumuona huku wakiwa na matawi ya miti.
Akitambulishwa
na umati mkubwa wa wananchi katika ofisi za mkoa wa chama hicho mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Geita Joseph Msukuma Kasheku amesema chama hicho hakika hakikukosea
kumteua Dr. Magufuli kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho kwa kuwa ni
kipenzi cha watanzania wote bila ya kujali itikadi za kivyama.
Akizungumza
wakati akiwashukuru,kuwaaga na kujitambulisha kwa wananchi waliokusanyika
katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoani Geita na hatimae vunja jungu katika
jimbo la chato mgombea urais wa CCM Dr.John Pombe Magufuli amekisukuru chama
hicho kwa kumuamini na kuongeza kuwa makundi ya wagombea wa nafasi ya urais
ndani ya chama hicho yamezikwa rasmi na limebaki kundi moja la umoja ni ushindi.
wakizungumzia
uteuzi wa Dr.Magufuli kugombea kiti hicho cha urais kupitia chama cha mapinduzi
baadhi ya wananchi wamesema tanzania imepata kiongozi atakayesaidia kuipeleka
tanzania katika nchi ya ahadi.
0 comments:
Post a Comment