Rais wa Kenya asema kuwa lengo la mazungumzo yake na Rais Obama ni Usalama na uhusiano wa Kibiashara wa nchi yake na si vinginevyo.
Rais Uhuru Kenyatta, alifahamisha kuwa kuimarishwa kwa usalama na kuongezwa kwa uhusiano wa kibiashara baina ya Kenya na Marekani itakuwa ndio masuala muhimu yatakayo jadiliwa kipindi rais Barack Obama atakapotembelea nchi za Afrika mashariki juma hili.
Pia watazungumzia kuhusu mapambano dhidi ya wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia,vyombo vya usalama nchini Kenya kupokea mafunzo na vifaa kutoka Marekani ,Uingereza na Israel.
Hata hivyo Kenya imewahi kupata mashambulizi makubwa kutoka kundi la kiislamu la Al-shabaab kutoka Somalia kwa muda wa miaka miwili mfululizo,ikiwa pamoja na mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu nchini Kenya karibu na mpaka wa Somalia.
Kenyatta, alisema kuwa natoa wito kwa makampuni mengi ya Marekani kufanyakazi pamoja na makampuni ya Kenya katika sekta za nishati, afya pamoja na miundombinu.
Kuanzishwa kwa ndege za moja kwa moja kutoka Kenya kuelekea Marekani pia itakuwa suala litakalo zungumziwa kufuatia udhaifu wa usafiri huo ambapo inapelekea hasara kubwa katika sekata ya biashara na Utalii,rais Kenyatta alisema.
0 comments:
Post a Comment