Image
Image

Rais wa Uturuki amepiga simu ya kuwafahamisha kuhusu mashambulizi ya kigaidi kwa viongozi wa nchi mbalimbali.


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amewafahamisha marais wa Ufaransa,Qatar na Saudi Arabia, kuhusiana na operesheni dhidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayoendelea nchini Uturuki.
Erdogan aliongea na marais kwa ufupi kupitia mazungumzo ya simu tofauti na Rais wa Ufaransa Francois Hollande, wa Qatar Emir Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani na wa Saudi Arabia Mfalme Salman bin Abdulaziz al-Saud.
Vyanzo vya habari vya rais vilifahamisha kuwa viongozi wa Ufaransa, Qatar na Saudi wamekuwa wakiunga mkono nchi ya Uturuki.
Rais pia aliwaambia viongozi kwamba machafuko yaliotokea nchini Syria pia kutishia usalama wa taifa la Uturuki.
Viongozi wa Kifaransa, Qatar na Saudi Arabia wametoa rambi rambi zao za dhati kwa nchi Uturuki juu ya tukio la kujitoa muhanga na kuua watu 32 katika eneo la Suruc katika mji wa Sanlurfa na mashambulizi mengine ya wanajeshi na polisi wa Kituruki katika siku za hivi karibuni.
Rais wa Ufaransa alifahamisha katika mazungumzo yake siku ya Jumatatu kuwa ameridhishwa na ushirikiano unaotolewa kwa nchi ya Uturuki katika kupambana na makundi ya kigaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment