Mchezaji namba moja wa tennis kwa
wanawake serena williams na mchezaji namba nne maria sharapova wametinga hatua
ya mzunguko wa tatu wa michuano ya wimbledon kwa ushindi wa seti mfululizo.
Willaims alimchapa timea babos
seti 6-3 6-1 huku kukiwa na joto kali na sasa anakutana na irina-camelia begu.
Wakati huo huo dada yaje serena,
venus williams na viktoria azarenka pia walifanikiwa kusonga mbele lakini
mchezaji namba saba kwa ubora ana ivanovic akatolewa kwenye michuano hiyo.
Kwingineko meneja wa timu
ya soka ya wanawake ya uingereza Mark Sampson amesema uingereza wanapaswa
kupokelewa nyumbani kama mashujaa pamoja na kutolewa kwenye michuano ya kombe
la dunia la wanawake baada ya kupokwa kichapo cha goli 2 kwa 1 kutoka kwa
japan.
Uingereza walijitahidi kuwazuia
mabingaw watetezi wa kombe hilo japan mpaka dakika ya 90 kabla ya beko laura
bassett kujifunga kwenye dakika za nyongeza.
Simpsom alisema inahuzunisha sana
lakini bado timu hiyo imeonesha uimara na ushujaa mkubwa kwani imeweka historia
ya kutinga nusu fainali za michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa
kwake.
Na
katika dondoo za usajili bayern munich ya nchini ujerumani imemsajili kiungo
wa Shkhtar Doneitsk Mbrazil Douglas costa kwa dau la paundi milioni 21.
Kusajiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24
kunaongeza uwezekano wa kiungo bastian shwensteiger kuhamia Manchester United.





0 comments:
Post a Comment