Image
Image

SERIKALI yaombwa kutazama na kutatua mahitaji ya watu wenye Albinism Nchini.


Watu wenye Albinism wilayani Mufindi  wameiomba serikali kutazama mahitaji yao ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika maisha ikiwemo ya maradhi ya ngozi pamoja na macho  yanayosababishwa na mionzi ya jua.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Albinism wilayani humo Bwana ANDREA KIWELU amesema watu wenye ulemavu wa ngozi wanaishi katika mazingira magumu ikiwemo kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka.

Watu hao wenye albinism wamesema hayo wakati wakipokea mafuta ya kusaidia kupunguza madhara ya mionzi ya jua kutoka kwa Mkurugenzi wa asasi isiyo ya serikali ya Mufindi Vijana kwa Maendeleo Bwana COSATO CHUMI.

Akikabidhi mafuta hayo ameitaka serikali na mashirika binafsi kusaidia upatikanaji wa mahitaji ya watu hao kwani licha ya kupambana na mauaji ya wenye albinism pia watu hao wanayo mahitaji mbalimbali, hivyo serikali itazame namna ya kuisaidia zaidi jamii hiyo.

Mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi Bibi JOHARI CHOGA amesema kutokana na unyanyapaa wanaofanyiwa kwenye jamii wanayoishi imekuwa vigumu kwao hata kufanya biashara ndogondogo kwa kuwa wateja nao huwabagua, jambo ambalo limeifanya jamii hiyo kuishi maisha magumu na kukabiliwa na umaskini wa kipato.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment