Mkuu wa
operesheni wa (TRA) mkoani Tanga Bwana.Kaimukelwa Johansen amesema
uchunguzi uliofanywa umeonesha kuna shehena kubwa ya sukari kisiwani Zanzbar
iliyotokea nchini Brazili ambayo imekuwa ikisafirsihwa katika baadhi ya mikoa
kupitia njia ya panya na bandari bubu ikiwemo mkoa wa tanga ambayo inauzwa
maeneo mengi.
Kwa
upande wake meneja wa forodhwa mkoani tanga Bwana. Pius Kibahila amesema hii ni
mara ya pili kwa sukari kukamatwa kutoka Brazil ikiwemo ile ya awali
iliyokamatwa mwezi wa tano mwaka huu hivyo amewaomba wakazi wanaoishi
jirani na bandani bubu kutoa ushirikiano kwa kikosi cha polisi cha wanamaji au TRA
ili kudhibiti hujuma hizo.
Kufuatia
hatua hiyo mamlaka hiyo imetangaza vita kwa wafanyabishara wasiokuwa waaminifu
kuwa watataifisha vyombo vilivyohusika na hujuma za ukwepaji ushuru wa forodha
pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wanaofanya makusudi
kuzorotesha jitihada za serikali katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.
0 comments:
Post a Comment