Image
Image

Sisi aipongeza Italia kwa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugaidi.




Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, ameipongeza nchi ya Italia kwa juhudi zake katikamapambano dhidi ya ugaidi.
Sisi alitoa maelezo hayo siku ya Jumatatu alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa ItaliaPaolo Gentiloni.
Mkutano huo ulifanyika siku mbili baada ya shambulizi kutekelezwa dhidi ya ubalozi wa Italiaulioko katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri na kusababisha kifo cha mtu mmoja na uharibifu wa majengo.
Kundi la Ansar Bayt al-Maqdis lililokuwa na makao makuu yake katika eneo la Sinai, lilituma ujumbe kupitia akaunti ya mtandao wa jamii wa Twitter na kutangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Waziri Gentiloni alitoa maelezo na kuarifu kwamba shambulizi hilo lililolenga ubalozi lilitekelezwa pasi na mafanikio na haliwezi kuvunja mahusiano kati ya Italia na Misri.
Gentiloni pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shukry na kujadili masuala ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment