Carlos Tevez amerejea katika klabu yake ya zamani ya Boca Juniors iliopo nchini kwaoArgentina baada ya kutumia miaka 11 kucheza soka barani Ulaya… Tevez amepokelewa kishujaa na mashabiki na viongozi wa klabu hiyo katika utambulisho rasmi wa kurejea Klabuni hapo.
Nyota huyo wa
Argentina aliyetumia zaidi ya miaka kumi kucheza soka barani Ulaya katika
vilabu mbalimbali ikiwemo Manchester United, Manchester City na Juventusametambulishwa
mbele ya mashabiki katika Uwanja wa Bombonera Stadium ambao unatumiwa na klabu hiyo kama
Uwanja wa nyumbani.
Carlos Tevez ameichezea Boca Juniors kuanzia mwaka 2001 hadi 2004 na kutimkia klabu
ya Corinthians ya Brazil na baadae akaelekea zake Ulaya. Tevez pia amecheza mechi 72 na timu ya taifa ya Argentina na kuifungia mabao 13, amecheza kombe la dunia
mwaka 2006 na 2010 lakini pia amewahi kutwaa medali ya dhahabu ya Olympic mwaka
2004.
Carlos Tevez na Raisi wa klabu ya Boca Juniors Daniel Angelici
Ada ya uhamisho
kutoka Juventus kwenda Boca Juniors haijatajwa na Klabu hiyo lakini
vyombo vingi vya habari barani Ulaya vinataja kufikia pound milioni 4.6.
Nyota wa soka
wa zamani Diego Maradona wa tatu kutoka kushoto akiwa anaangalia utambulisho wa
mchezaji huyo.
Nimekuwekea
video ya utambulisho wa Tevez hapa mtu wangu.
Bofya Hapa Kuona Pia usisahau ku Like ukurasa wetu hapo juu ili kuweza pia kupata habari KemKem.
Bofya Hapa Kuona Pia usisahau ku Like ukurasa wetu hapo juu ili kuweza pia kupata habari KemKem.
0 comments:
Post a Comment