Image
Image

TFF yalia na viongozi wa klabu kutotoa ushirikiano

KAIMU Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jemedari Said amelalamikia kitendo cha viongozi wa klabu za Ligi Kuu kutokuwa na ushirikiano katika masuala muhimu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Said alisema viongozi wengi wa klabu za Ligi Kuu wamekuwa wa kwanza kulalamika na kuitupia lawama TFF wakati wao wenyewe si watu wa kutilia maanani kwenye masuala muhimu.
“Imekuwa kawaida kwa viongozi wa klabu likitokea jambo ni wa kwanza kulaumu TFF wakati wao kuna masuala muhimu ni wagumu kuyatekeleza hata kama yanahitaji jambo kidogo sana,” alisema.
Akifafanua kauli hiyo, Said alisema imepita zaidi ya wiki viongozi wa klabu waliombwa majina ya makocha wao wa makipa kwa ajili ya kozi ya Fifa lakini mpaka kufikia jana ni klabu mbili pekee za JKT Ruvu na Majimaji ndizo zilizoitikia mwito.
“Unaona hii kozi ni makocha wa makipa itaendeshwa na Fifa mwishoni mwa mwezi huu, taarifa viongozi wote wanazo lakini kuinua simu tu au kunitumia ujumbe kwamba timu fulani kocha wetu ni fulani hawawezi kufanya hivyo… “Hivi hapa ndio nina kazi ya kuwapigia simu mmoja mmoja kuwauliza kuhusu jina la kocha wao wa makipa, kitu muhimu kama hiki lakini hawakitilii maanani… “Kwa mfano kama Yanga tunajua kwamba kocha wao wa makipa ni Pondamali (Juma) taarifa walikuwa nayo kama zilivyo klabu nyingine, lakini leo (jana) mapema asubuhi niliwapigia simu wanipe jina la kocha wao lakini mpaka saa nane hii mchana nazungumza na wewe hawajanipa, ugumu uko wapi,” alisema.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment