Image
Image

TRA yaanza kutumia sheria mpya kukusanya mapato.

Baada ya kutunga sheria mpya ya Ongezeko la Thamani VAT, ya 2014 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, imeanza kutekeleza sheria hiyo huku ikiwataka walipa kodi kuisoma na kuifuata bila shuruti.
Afisa kodi mwanadamizi wa TRA, Donasian Assey amesema serikali imefanya mabadiliko ya sheria kutokana na iliyyokuwepo kuwa na upungufu mkubwa na kuikosesha serikali mapato.
Assey amesema sheria mpya imefafanua jinsi ya ulipaji kodi na watu wanaotakiwa kulipa wakati mwaka 1997 ilikuwa haielezi na kuainisha maenep ya kusamehewa kodi.
Naye Afisa TRA Bw. Peter Kiatu amesema kutokana na sheria iliyofutwa kuwa na upungufu serikali ilitenga kukusanya kodi asilimia sita ya pato la taifa kwa mwaka badala yake ilikusanya asilimia 4.8 hivyo ilikuwa ikipoteza mapato na kupata hasara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment