Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa
Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili, Julai 19, 2015), Waziri Mkuu
Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa
Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia
wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati
wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika
mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua
kutoka kwenye umaskini.
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la Katavi wawe makini
katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu
wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya
wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele
kumuenzi Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hata atakapokuwa amestaafu kwani
bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili
ya mapumziko mafupi.
Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya
Chama cha Mapinduzi (CCM).
0 comments:
Post a Comment