Twitter kuanza kulinda hatimiliki za ujumbe wa watumiaji wake mtandaoni.
Mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter umeanza kuleta mabadiliko makubwa kwa ajili ya kulinda hatimiliki za watumiaji wake.
Mojawapo ya mabadiliko hayo ni kuleta suluhisho kwa matumizi ya ujumbe wa mtumiaji maalum unaoweza kunakiliwa na kurudiwa na watumiaji wengine mtandaoni bila idhini.
Twitter sasa itaanza kufuta ujumbe wa aina yoyote utakaogunduliwa kupeperushwa na mtu asiyekuwa mmiliki wa akaunti iliyopeperusha ujumbe huo mwanzoni.
Vile vile Twitter pia itafanyia uchunguzi ujumbe wowote utakaoripotiwa kunakiliwa na baadaye kuchukuwa hatua kama ipaswavyo.
0 comments:
Post a Comment