‘’Nitafungwa jela kwa sababu ya kutusiwa... na bado kombe la dunia litafanyika nchini humu’’ Alisema pingpong katika ukurasa wake wa twitter.
Mchezaji wa Zenit St Petersburg na Brazil, Hulk, alisema kuwa ubaguzi na matusi umekithiri katika mechi nyingi za ligi hio na kwamba huenda ikawa changamoto kubwa kwa kombe la dunia, miaka mitatu ijayo. Aliongeza kuwa ‘’lItakuwa swala la kuhuzunisha kama matusi haya yatedendelea katika kombe la dunia.’’
Shirika la kandanda la Ghana limesema kuwa kutokana na kisa hicho cha Frimpong, waliotoa matusi wanafaa wachukuliwe hatua kali na shirika la Russia, UEFA na FIFA.
Mchezaji wa Ivory Coast Yaya Toure amesema kuwa wachezaji wa Afrika huenda wakajiondoa katika michuano hio kama hawatakuwa na imani ya kukoma kwa tabia hii.
Hii ni baada ya Toure kutukanwa na mashabiki wa CSKA Moscow katika mchuano wa Kombe la timu bora Uropa kati ya timu hii na timu yake, Manchester City. Kutokana na haya, CSKA Moscow ililazimishwa na FIFA kucheza awamu ya pili bila mashabiki.
Repoti iliyotolewa na Fare Network na Kampuni ya Moscow Sova Center ilionyesha kuwa kumekuwa kuna recodi ya kesi 99 za matusi na kesi nyingine 21 zilizofichwa katika misimu yote miwili iliyopita, recordi inayotupiliwa mbali na serikali ya Urusi.
Hata hivyo baada ya Alexei Sorokon anayepanga michezo hiyo ya Kombe la dunia 2018 kuhojiwa kutokana na maoni ya Hulk, alisema kuwa ‘’tunakubali kuwa kuna tatizo hili lakini huwa haitokei Urusi pekee bali hata katika nchi zingine.’’
Kwa mfano, katika mwaka wa 2011, Roberto Carlos akiichezea timu ya Anzhi Makhachikala alitupiwa ngozi za ndizi na mashabik wa Zenit lakini hivi karibuni, Dani Alves alipitia haya akiwa Uispania, Didier drogba na Emmanuel Ebuoe wakiwa Uturuki na Kevin Constant na Nigel De Jong wakiwa Italia.
Pia, timu ya Uingereza wenye chini ya miaka 21 wakicheza na Serbia, mwaka wa 2012 ilifuatwa na vita kati ya mashabik baada ya wachezaji weusi wa Uingereza kutusiwa.
Mashabik wa Zenit walisajili pendekezo la ‘’section 12’’ ambayo inasisitiza kuwepo kwa timu ya watu wasio weusi tupu, bado kuna mashabik wa kutoka Ugerumani na Italia waliobado na matusi.
Ubaguzi huu na matusi umeskika na wanahabari katika mechi za timu ya kigerumani Energie Cottbus kwa mfano ambapo mashabik wa timu ya Lazio ya Roma wanajulikana kwa upendeleo wao.
Sorokon aliongeza kuwa si vizuri ‘’kuchukua visa vya ligi ya Urusi na kuvichukua kama visa vitakavyotokea katika kombe la dunia kwa sababu kombe la dunia ni tofauti kabisa na ina mashabik tofauti kwa hivyo si lazima visa vitatokea katika michuano hayo. ‘’
Visa katika kombe la dunia mwaka wa 2014 nchini Brazil ni kama kile kilichotokea katika mchuano kati ya Ugerumani na Ghana ambapo shabiki mmoja alikimbia na kuingia uwanjani , mashabika wa Mexico, pamoja na kelele za matusi kutoka kwa mashabiki wa Croatia na Urusi.
Jeffery Webb aliyekua akismamia sekta ya kupunguza visa vya aina hii alikubali kuwa wangefanya zaidi ili kurekebisha haya akiongeza kuwa katika kombe la dunia litakalo fuata, kutakuwa na maafisa 3 katika mechi zote kutambua watu wenye tabia ya aina hii. Webb ni mmoja wa walitajwa kama wafisadi.
Atakayechukua kazi hio baada yake atakuwa na kazi ya kuhakikisha ubaguzi wa aina hii unasitishwa kutoka miongoni mwa mashabiki wa Urusi na kwingineko.
0 comments:
Post a Comment