Image
Image

Ugiriki:Wakopeshaji wanataka kutudhulumu

Waziri wa fedha nchini Ugiriki ametoa taarifa siku moja kabla ya kuandaliwa kwa kura ya maoni juu ya mpango wa kulipa deni lake.
Kwenye mahojiano na gazeti la El Mundo nchini Uhispania Yanis Varoufakis aliwalaumu wakopeshaji wa nchi kwa kile alichokitaja kuwa ugaidi akisema kuwa wanataka kura ya ndio ili waweze kuidhulumua Ugiriki.
Aliongeza kuwa mabenki nchini Ugiriki yatafunguliwa siku ya Jumanne bila kujali matokeo ya kura hiyo.
Mapema pande mbili kwenye kura hiyo ya maoni zilimaliza kampeni zao kwa mikutano mikubwa.
Waziri mkuu Alexis Tsipras amesema kuwa kukataa kura hiyo kutamwezesha kupata makubaliano mazuri na wakopeshaji wa nchi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment