Image
Image

Ujenzi wa kituo cha kupokelea gesi SOMANGA wakamilika.

Ujenzi wa kituo kikuu cha kupokelea gesi asilia cha SOMANGA mkoani Lindi, umekamilika kwa kiwango kikubwa tayari kwa kupokea gesi kutoka vyanzo mbalimbali kabla ya kusafirishwa kwa ajili ya matumizi mengine.
Akizungumzia kukamilika kwa kituo hicho, ambacho kitakuwa kikipokea gesi asilia kutoka chanzo cha  kuzalisha gesi cha  MADIMBA  mkoani MTWARA na SONGOSONGO  mkoani LINDI , kaimu meneja wa kampuni ya kusambaza gesi  GASCO Mhandisi KAPUULYA MUSOMBA amesema kituo hicho kitatumika kusafisha gesi hiyo kabla ya kupelekwa jijini DSM kwa matumizi ya nishati.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TPDC MICHAEL MWANDA amesema kukamilika kwa mradi huo kunadhihirsha kutekelezwa kwa vitendo  mpango wa serikali unaolenga kuwapatia watanzania huduma ya nishati ya umeme kwa bei nafuu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment