Watu
wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa baada ya
Treini ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don’t Worry lililokuwa
likitokea mjini Tabora kuelekea ufuruma uyui
mkoani humo lilipofika eneo
la kuvuko cha reli eneo loa malolo manispaa ya Tabora katika kile kilichodaiwa
kuwa ni uzembe wa dereva.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wamesema
kuwa, dereva aliyekuwa katika mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia
eneo hilo inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata
kona ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na kukutoa paa
lote la juu la gari.
Aidha
kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina
msaidizi Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za
usajili T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva
aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya kusababisha ajali
hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya rufaa na mkoa wa Tabora.
Viongozi
wa shirika la reli waliofika katika
eneo la ajali hiyo wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani
kwani shirika la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini
kutokana na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama
hiyo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment