Umoja wa mataifa watoa msaada wa chakula Yemen.
Mashirika ya vyombo vya habari yametaarifu kuwa:
Shirika la chakula duniani la umoja wa mataifa limeanza kutoa misaada ya chakula kwa zaidi ya watu 340,000 katika maeneo ya kusuni mwa mji wa bandari ya Aden nchini Yemen.
Mkurugenzi wa shirika hilo amesema kuwa "tunatoa changamoto kwa wale wasiotaka kutoa misaada kwa watuwanaolala njaa bila ya msaada wa chakula.”
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa karibuni watu 4,000 wameuawa nchini Yemen kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa na makundi ya kigaidi kipindi cha mwezi Machi.
Takriban wa watu milioni 21, ambapo ni sawa na asilimia 80 ya idadi ya watu, wapo katika hali ya kuhitaji misaada ambapo miongoni mwao ni milioni 13 wana uhaba wa chakula.
Wafanyakazi wa utoaji wa misaada walianza kugawa vyakula miezi miwili iliyopita.
Shirika la chakula lilifahamisha kuwa:
Vyakula hivyo vilivyotolewa ilikuwa ni pamoja na unga wa ngano, kunde na mafuta ya kupikia katika maeneo kadhaa ya bandari ya Aden.
0 comments:
Post a Comment