Watu zaidi ya 500 wameripotiwa kuwekwa kwenye karantini baada ya kesi mpya za Ebola kugunduliwa tena upya katika mji wa Tonkolili ulioko kaskazini mwa Sierra Leone.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mkuu wa kituo cha kudhiti Ebola (NERC), watu hao watatengwa kwa muda wa siku 21, na chifu wa eneo hilo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kushindwa kutahadharisha maafisa wa afya.
Kati ya watu hao zaidi ya 500 waliotengwa, wapo wafanyakazi 30 wa huduma za afya kutoka hospitali moja ya mji ambapo walikuwa wakimhudumia mgonjwa mmoja wa Ebola kabla ya kufariki.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba mgonjwa huyo alipelekwa kwa mganga wa kienyeji kwanza badala ya kufikishwa hospitalini punde tu alipoanza kuonyesha dalili za virusi vya Ebola.
Viongozi wametoa tahadhari kwa wananchi wa Sierra Leone kuzingatia hatua za maafisa wa huduma za afya ili kuepukana na janga la Ebola.
0 comments:
Post a Comment