Image
Image

UNFPA yasaidia wanawake wajawazito nchini Yemen.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA limeanzisha mradi wa kusaidia wanawake wajawazito nchini Yemen ilikuwasaidia kujifungua kwa njia salama, na kupambana na ukatili wa kijinsia.
Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNFPA imesema miongoni mwa watu milioni 21 walioathirika na mzozo nchini Yemen, 472,000 ni wanwake wajawazito, huko 70,000 wakiwa hatarini ya kupata shida wakati wa ujauzito wao na kuhitaji upasuaji.
Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Hymyar Abdulmoghni, Mkwakilishi msaidizi wa UNFPA nchini Yemen amesema changamoto kubwa ilikuwa ni kuwafikia wanawake hawa.
 Tunaweza kusema kwamba tumewafikia wanawake 230,000 kwenye majimbo hususan kusini mwa nchi ambapo mapigano yanaendelea. Sasa tunalenga majimbo mengine kaskazini mwa nchi, na tukijaliwa mwisho wa wiki tutakuwa tumefikia zaidi ya wanawake 300,000 »
Msaada uliosambaza na UNFPA ni pamoja na vifaa vya kuzalisha kwa dharura na kuhudumia watoto wachanga. Misaada mengine imesambazwa na UNFPA ikiwemo vifaa vya afya ya uzazi, pia nguo, taulo, sabuni, chanjo na kadhalika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment