Vijiji vya Upper River vyakumbwa na mafuriko nchini Gambia.
Nchi ya Gambia imekuwa ikikumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha tangu siku ya Jumapili.
Mafuriko hayo yameripotiwa kuathiri vijiji vya Sandu na Wuli vilivyoko katika eneo la Upper River nchini Gambia.
Barabara kuu za kuunga miji mbalimbali zimeripotiwa kuharibiwa huku usafiri ukisitishwa kwa muda.
Wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa nchini Gambia wametoa tahadhari ya uwezekano wa mvua kubwa kuendelea kunyesha katika siku zijazo.
Ingawa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mali uliosababishwa na mafuriko hayo, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na vifo vyovyote vilivyozuka.
0 comments:
Post a Comment