Katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN)
Ban Ki-moon, alionyesha huzuni kubwa kwa nchi ya Uturuki kufuatia vifo
vinavyoendelea kutokana na wimbi la mashambulizi.
Msemaji wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa
alifahamisha kuwa "alitoa rambirambi zake za dhati kwa serikali na watu wa
Uturuki kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya vurugu za kigaidi"
Uturuki inakabiliwa na mfululizo wa
mashambulizi na kundi la Daesh na wanamgambo wa serikali ya kikurdi.
Tangu kuanza kwa mashambulio haya
watu 32 wamepoteza maisha kusini mwa mji wa Sanliurfa Julai 20
mwaka huu katika shambulio la kujitoa mhanga kwa mtu wanaohusishwa na Daesh.
Uturuki imefanya operesheni na
kuwakamata wanachama wa makundi yote mawili Daesh na PKK na pia
kufanya mashambulizi ya mabomu ya anga katika maeneo ya Syria na İraq.
0 comments:
Post a Comment