Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Bara
wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan, wakati
wa mwendelezo wa uchambuzi wa maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na
madiwani wa mwaka 2015.
“Tume ya uchaguzi isimamie vizuri gharama za uchaguzi na ziwe wazi ili kuepusha migogoro kwenye vyama,” alisema.
Alilishauri Jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa askari wao kwa ajili
ya shughuli za uchaguzi ili kuepuka vitendo vya uonevu ambavyo vinaweza
kujitokeza.
Alisema vyombo vya ulinzi na usalama visitumike kukandamiza wagombea na wafuasi wa chama chochote cha siasa.
Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura, aliitaka
Nec kuhakikisha inadhibiti matumizi ya magari ya serikali kutumiwa na
vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi.
Kila chama kinatakiwa kutumia magari yake kuendesha shughuli zake za kampeni wakati wa uchaguzi.
Vyama hivyo pia viliishauri Nec kutopeleka masanduku ya kura kwenye
kambi za jeshi badala yake wanajeshi wapige kura katika vituo vya
kupigia kura vilivyopo uraiani, kinyume chake ni kuwanyima uhuru.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alisema wao hawaruhusu
vyombo vya uchaguzi kupiga kura kwenye kambi za jeshi na kuahidi
kulifuatilia suala hilo.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mtungi (pichani),
aliitaka Nec kuviwezesha vyama vya siasa kwenye uchaguzi ili viweze
kuwahudumia mawakala wao kutokana na vingine kupata ruzuku na vingine
kukosa.
Jaji Lubuva alisema mapendekezo hayo yatafanyiwa marekebisho kabla ya kusaini maadili hayo.
0 comments:
Post a Comment