Msimamo huo ulitolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Amina
Makilagi, alipoulizwa swali na waandishi kuhusu msimamo wa mwenyekiti
huyo, baada ya kutoa tamko la jumuiya hiyo la kumpongeza Magufuli.
Sophia Simba mwishoni mwa wiki alijitokeza hadharani akiwa na
wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya (CC) ya chama hicho, Adam Kimbisa na Dk.
Emanuel Nchimbi, kwamba hawaungi mkono na sio sehemu ya maamuzi
yaliyotolewa na CC juu ya majina matano ya wagombea urais yaliyopelekwa
katika Halmashauri Kuu ya (NEC)
Majina hayo mbali na Magufuli ni ya Dk. Asha-Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali.
Wajumbe hao walisema hawajakubaliana na maamuzi hayo kwasababu
hayakufuata Katiba na kanuni za chama hicho, kutokana na CC kutopokea
majina yote ya walioomba uteuzi na kuwa ni kinyume na kanuni.
“Kwenye hili tamko tupo pamoja na Mwenyekiti wetu (Sophia Simba) na
kabla sijaja hapa tumekutana nilikuwa naye asubuhi, haya yote
niliyozungumza hapa tumeyatengeneza kwa pamoja na tulichokubaliana ni
kwamba nije hapa tuzungumze,” alisema Makilagi.
Aidha alisema hivi karibuni wameandaa hafla ya kumpongeza Samia
Hassan Suluhu kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza, na Simba atajitokeza na
kuzungumza na wananchi.
“Tutaandaa kitu kikubwa tu ambacho yeye (Sophia) atatoka na
atasimama na kuzungumza na wananchi tukiwa tumeandaa kazi ndogo ya
kumpongeza Mama Samia Suluhu,” alisema Makilagi.
Awali akisoma tamko la pongezi, Makilagi alisema jumuiya
inampongeza kwa dhati na kuahidi kumuunga mkono Dk. Magufuli kuhakikisha
chama kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Alisema katika Taifa la Tanzania mchango wa wanawake ni mkubwa
sana na kumpongeza Dk.Magufuli kwa kumteua Suluhu kuwa mgombea mwenza.
0 comments:
Post a Comment