WAKAZI milioni 2.9 mkoani Dar es Salaam wanatarajia
kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpigakura kupitia Mfumo wa
Kielektroniki (BVR) huku wageni wakipigwa marufuku kushiriki katika mchakato
huo.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa mkoa huo, Said Meck Sadiki
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya maandalizi ya
uandikishaji huo.
Sadiki alisema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)inaendelea na shughuli za
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika mikoa mbalimbali na kazi
ya uboreshaji wa daftari hilo la kudumu la wapigakura inatumia teknolojia mpya
ya mfumo wa uandikishaji.
Alisema, mfumo huo unatumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
"Mkoa wa Dar es Salaam tunatarajia watu milioni 2.9 wawe wamejiandikisha
katika daftari hilo la kudumu kuanzia Julai 22, mwaka huu hadi Julai 31 kwa
mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi," alisema.
Sadiki alisema, katika mkoa huo maandalizi tayari yamefanyika kwa halmashauri
zote tatu ambayo yatasaidia kufanikisha zoezi hilo kikamilifu.
Wakati huo huo, Mkuu huyo aliwataka wakazi wa mkoa huo kutojiandikisha mara
mbili kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tume ya Uchaguzi nchini.
"Pia raia wa kigeni ambao wapo Dar es Salaam nao ni marufuku kushiriki
katika zoezi hilo, wakae katika mji salama, lakini wasijihusishe kwenda
kujiandikisha ni marufuku kwao," alisema Sadiki.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment