Mbunge wa Kahama anayemaliza muda wake kupitia chama cha mapinduzi Mh.CCM
James Lembeli Ametangaza rasmi hivi leo kukihama chama hicho na kujiunga na
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Kuhama chama hicho cha CCM Lembeli ni kufuatia siku chache za
kuwepo kwa taarifa kuwa hatoendelea kuwa mbunge kupitia CCM na kudai kuwa
nafasi hiyo atairejesha kupitia chama kingine ambacho hakuwa wazi kukisema na
kusema kuwa hatorudi nyuma na msimamo wake.
Baada ya uamuzi wake, watu mbalimbali, wakiwamo maofisa wa
Serikali na wafanyabiashara waliahidi kumsaidia hata nguvu ya kifedha,
wakimtaka atengue uamuzi wake achukue fomu katika Jimbo la Kahama Mjini.
Alisema hawezi kukiuka masharti ya kimila kwa kuwa yeye ni mtoto
wa chifu. Mtoto huyo wa Chifu Daud Lembeli alisema kabla ya kutoa uamuzi huo
alikaa na mama yake mzazi, Maria Kalembo kuanzia saa 10 jioni hadi saa nane
usiku akizungumzia suala hilo hadi walipokubaliana.
Alisema baada ya mama yake kukubali na kutoa baraka za kuhama CCM,
alipigiwa ngoma za kimila za Waswezi, ambazo hutumika kutoa baraka katika imani
za kichifu akisema ndizo zilizohitimisha fursa za kugombea kwake ubunge kupitia
chama hicho.
“Najisikia amani kubwa kuondoka CCM, kabla sijachukua uamuzi huu
nilikuwa nikiishi kwa presha, hivi sasa nipo huru, niacheni tu kama ni ubunge
sikuzaliwa nao na unaweza kuishi bila ubunge na maisha yakawa mazuri,” alisema
Lembeli.
Ilivyokuwa
Juzi, Lembeli alifika katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Kahama na
kutangaza kuwa hawezi kugombea kupitia chama hicho kwa kuwa kimejaa rushwa na
matukio ya wagombea kugawa kadi kwa wanachama ili wachaguliwe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Mabala Mlolwa alielezea
kusikitishwa na uamuzi huo wa Lembeli kuamua kuhama bila kushauriana na uongozi
wa wilaya.
Alisema CCM inatambua mchango mkubwa aliotoa katika miaka 10 ya
uongozi wake na imeshangazwa na tukio hilo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja alisema pamoja
na kulisikia suala hilo, hivi sasa yupo mapumzikoni kisiasa kutokana na dhoruba
kubwa ya kitaifa waliyoipata katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais.
“Niacheni kwanza nipumzike suala hilo nalisikia lakini muda mwingi
sikuwapo. Najua suala la Lembeli kuhama litaibomoa CCM Kahama, ataondoka na
wengi lakini mimi sizungumzi lolote juu ya hilo,” alisema Mgeja.
Sikiliza hapa akizungumza juu
ya kukihama chama hicho leo.
0 comments:
Post a Comment