Asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi
zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia 12.4
wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75 na
asilimia 90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na umri wa chini ya
miaka 40.
Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta wakati
akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza
magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na
tezi dume unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC)
uliopo mjini Nairobi.
Rais Kenyatta alisema Ripoti ya saratani iliyotolewa mwaka 2014 na Shirika
la Kimataifa la kutafiti saratani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani
(WHO) ilionyesha takwimu mpya za saratani zinaongezeka kila mwaka na
kwa upande wa Afrika vifo vingi vinatokana na saratani ya mlango wa
kizazi.
“Watu wanapoteza maisha na kuugua saratani kutokana na kutokuwa na
uelewa wa ugonjwa huo, kutokuchukua hatua za mapema na watu kutambulika kuwa
na ugonjwa wa saratani wakati umefikia hatua ya mwisho kutokana na hili
tutaendelea kuwa na wagonjwa ambao wanapata maumivu, wanashindwa kupata
matibabu kwa wakati na uangalizi wa karibu katika bara letu”.
Ni lazima tuhakikishe jamii inajulishwa kuhusu ugonjwa wa saratani
na kubadilisha aina ya maisha tunayoishi kama watu wataacha kuvuta
sigara, watakula vyakula vyenye afya, atapunguza kunywa pombe na kufanya
mazoezi mara kwa mara tutakuwa tumezuia asilimia 40 ya saratani”, alisema.
Aidha Mhe. Rais Kenyatta alisema katika bara la Afrika ugonjwa wa
saratani siyo moja ya agenda inayopewa kipaumbele katika masuala ya afya
ukilinganisha na magonjwa mengine kama ya kuambukiza lakini
sasa ili kupambana na saratani kunatakiwa kuwa na mikakati kwa nchi chache
ambazo zitaweza kukutana na kufanya utafiti na kutoa matibabu ili
kuzuia watu wasife na hivyo kuokoa maisha katika hatua ya mwanzo ya ugonjwa.
Mhe. Rais Kenyatta alimalizia kwa kusisitiza kuwa watu wanahitaji kupata chanjo ya hepatitis ambayo inazuia saratani ya Ini na Human Papilloma Virus (HPV) inayozuia saratani ya mlango wa kizazi ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya saratani katika bara la Afrika.
Akiwakaribisha wake wa marais na wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria mkutano huo Mke wa Rais wa Kenya Mhe. Mama Margaret Kenyatta alisema ni muhimu wadau hao wakaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na magonjwa hayo ya saratani.

Mhe. Mama Kenyata ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la wake wa
marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni
mlango wa kizazi, matiti na tezi dume kwa mwaka 2015 – 16 alisema wamefanikiwa
kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa ya saratani wanachotakiwa kukifanya
hivi sasa ni kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze kujichunguza
dalili za awali za saratani na kutibiwa kuzuia kwani saratani nyingi
zikigundulika mapema zinatibika.
Alisisitiza, “Tunatakiwa kuwashawishi viongozi, Serikali na sekta
binafsi na taasisi zisizo za kiserikali kuchukua hatua za lazima ili kuweza
kukabiliana na saratani na hivyo kuokoa maisha ya watu wetu”.
Kuhusu ulaji wa vyakula alihimiza ni muhimu waafrika wakaangalia
maisha ya zamani na kurudi nyuma kwa kuanza kula vyakula vya asili
na kuacha kula vyakula vilivyosindikwa hasa kwa vijana”
Mkutano huo wa siku tatu wenye kauli mbiu ya wekeza kuokoa maisha: wajibu wa ushirikiano wa sekta binafsi ulihuhuriwa na wake wa Marais kutoka nchi 12 akiwemo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete.

0 comments:
Post a Comment