Siku chache baada ya chama cha mapinduzi
CCM kumpata mgombea wake wa katika kiti cha urais,baadhi ya wananchi na
wananchama wa chama hicho wameutaka uongozi wa juu kufanya maridhiano na
makundi ambayo yanaonekana kutoridhika na mchakato ili kujenga umoja ndani ya
chama utakaokisaidia chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi
mkuu wa october 2015.
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi na wananchi hususani wakazi wa Dar es Salaam wameonesha kuridhishwa
na mcahakato huo uliomteua Dr.John Pombe magufuli kupeperusha bendera ya CCM katika
uchaguzi mkuu wa October na kuutaka uongozi wa juu wa chama hicho kufanya
maridhiano kumaliza mivutano ya ndani na nje ya chama ili kuwe na nguvu moja ya
kumnadi mgombea wao pale kipyenga cha kampeni kitakapopulizwa.
Aidha wakazi wa jiji la Dar es salaam nao wamepewa
wito wa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftari la kudumu la
kupiga kura pale zoezi hilo litakapoanza jijini dar es salaam ili kupata fursa
ya kupiga kura kama haki ya msingi ya raia zoezi litakalosaidia kuwaondoa madarakani
viongozi wasiotekeleza matakwa ya wananchi na kuwaweka madarakani viongozi
waadilifu watakaosaidia kusukuma gurumu la maendeleo baaada ya uchaguzi mkuu wa
October 2015.
0 comments:
Post a Comment