Vyama viwili katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu CCM pamoja na UDP vimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wapatao 10 kutimkia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kuchoshwa na uongonzi wa vyama hivyo.
Akiwataja majina madiwani hao Katibu Mwenezi Chadema wilayani Bariadi Martine Mogani, alisema kuwa kati ya hao, watatu ni kutoka CCM na saba kutoka UDP ambao ni Benjamini Matondo (UDP) Nyakabindi, Shiwa Danhi (UDP) Sapiwi na Gulya Nyembe (UDP) Ihusi.
Wengine ni Ruta Mahagija (CCM) Dutwa, Nhandi Madede (UDP) Ikungulipu, Matalu Mongobusia (UDP) Mwaubingi, Andrea Henoka (UDP) Nkindwabiye, Juma Nengelo (CCM) Somanda pamoja na Masunga Ngagani (UDP) kutoka kata ya Sakwe.
Mtia nia
nafasi ya Ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi Seni Silanga kupitia
Chadema, akiongea na mamia ya wananchi katika kata ya Dutwa wakati wa
kutambulishwa kwa madiwani 10 waliojiunga na chama hicho.
0 comments:
Post a Comment