Maiko litanda aliyekuwa
kiongozi wa kundi la M4U, lililokuwa
likimuunga mkono mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.Edward Ngoyai Lowasa amekuwa mmoja wao wa kukihama
chama cha CCM na hivyo kuhamia Chadema.
Sababu za kinaga ubaga alizo
zisema mpaka kumpelekea kuondoka kwenye chama na kundi lake ni kwamba maamuzi
yaliyofanywa kwa manufaa ya wachache ndani ya CCM kwa kumkata jina Bw.Edward
Lowassa ndio sababu kuu haswa na kusema kwamba huo simoto wa Gesi unaozimika gafla
kwani bado wanayo imani na safari yao ya matumaini ambayo inaendelea na sasa
inahamia chama cha democrasia na maendeleo chadema.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa M4U
anasema zaidi ya vijana 100 wamekwisha kujiunga na CHADEMA huku uongozi wa chadema
mkoa ukiwahakikisha kuwafikisha salama katika safari ya matumaini.
Katika hatua nyingine chama cha ACT
Wazalendo kimepokea wanachama 7 kutoka
vyama vya upinzani ambapo wanadai kuondoka kwao kunatokana na viongozi wa vyama
hivyo kuwa na ombwe la uongozi huku
vingine vikiendeshwa kwa ukanda.
Vugu vugu hili linakuja siku
kadhaa zikiwa zimesalia kabla ya UKAWA kumuweka wazi mgombea wao wa urais huku
kukiwa na Fununu kwamba huenda mmoja wa
vigogo wa CCM yuko mbioni kujiunga na umoja huo.
0 comments:
Post a Comment