Zaidi ya Waislam bilioni 1.5 duniani ambao
waliitekeleza ibada ya ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,
wamesaliwa na siku moja ili kukamilisha ibada hiyo na hatimaye
kusherehekea sikukuu ya Eid.
Mwezi wa Ramadhani huwa na nema kubwa kwa Waislam kwani huongeza
mapenzi baina ya ona huwezesha maksini, wasiojiweza, na yatima kusaidiwa
kwa kiasi kikubwa.
Pia huleta amani, upendo na ukaribu baina ya watu. Kuna mengi zaidi
ya kuyaelezea kuhusiana na mwezi huu ukiachana na hayo niliyoyataja.
Dhana na msingi mkuu wa kanuni za Kiislam ambazo zimetolewa kutoka klatika Quran na mwangaza wa Sunna na hadithi za Mtume ni kuhakikisha kuwa watu wanakua wenye furaha.
Ingawa suala la furaha kwa binadam ni tata sana, lakini Uislam
unawaamuru waumini wake kujifanyia matendo mazuri na kuzifanyia familia
zao, jamii zao, nchi zao na dunia nzima kwa ujumla.
Kauli mbiu ya wizara ya masula ya dini mwaka huu ni “kufanya mema”,
hivyo wizara hii imeelekeza nguvu zake kuhakikisha kuwa kauli mbiu hiyo
inatimizwa. Lengo kuu likiwa ni kuwawekea watu mazingira ya kufanya
matendo mazuri tu.
Jambo hili linafanywa kwa kufuata maamrisho ya Quran na mafunzo ya Mtume Muhammad kama isemavyo moja ya sura za Quran, Surat Al- asr “Kuamrishana kufanya mema”.
Tutakua naye Profesa Ramadhan Gozen ambaye ni mkufunzi wa idara ya Uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha Marmara.
Yafuatayo ndio maelezo aliyoyatoa mtaalamu wetu, profesa Gozen kuhusiana na mada yetu ya leo.
Jambo
la kwanza ambalo tunapaswa kulielezea hapa ni kuwa kufanya wema ni
fadhila. Tunaweza kuifupisha na kujadili jambo hili ambalo huchukua
maelezo mengi katika falsafa kama ifuatavyo.
Kwanza fadhila ya kufanya wema inajumuisha shughuli zote na
makubaliano ambayo watu hufanya. Hii inaweza kuwa na pande mbili upande
hasi na upande chanya.
Kwa upande chanya, kufanya wema au matendo mazuri huleta matokeo mazuri kwa mfanyaji na watu wote.
Hii
huwezeshwa na kuendelezwa kwa kuwasaidia wengine, kushirikiana katika
kazi, kuwafanyia wema majirani na mifano mingine kedekede ambayo huleta
faida kwa watu.
Upande mwingine una matendo mabaya ni kufanya mambo ambayo yatakuwa na madhara kwa mfanyaji na watu annaowafanyia.
Hatutakiwi kujipa madhara wenyewe au kuwadhuru wengine, kuiba mali za
watu, kuwaathiri watu kisaikolojia au kimwili na kutowasumbua wengine.
Kiukweli inakubalika kwamba hata kufanya kitendo kimoja tu ambacho kitaleta furaha kwa watu ni muhimu sana.
Moja ya malengo makuu ya Uislam ambayo kila mtu anakubaliana nayo ni kufundisha namna ya kufanya matendo mazuri.
Kwa maneno mengine ni kuwa Uislam umejitokeza kwa watu na namna zake
za kipekee, njia, namna na muongozo kwa watu.Kwa mfano matendo yote
yanayofanywa mwezsi wa Ramadhani yanadhihirisha jambo hili. Na lengo kuu
si mwezi wa Ramdhani bali kuishi kwa kufuata taratibu hizi katika
kipindi chote cha maisha.
Hata hivyo mjadala mkubwa unazuka linapokuja suala zima la utekelezaji.
Na hili husababishwa pengine na mana ya kufanya matendo mazuri inayotolewa au namna inavyotekelezwa.
Je
walimu kujitolea kufuındisha wanafunzi, matajri kutoa nkuwasaidia
masikini(kidini huitwa Zaka au sadaka) au kuisaidia nchi iliyokumbwa na
tetemeko inatosha kuwa matendo mema?
Na j eni matendo kama kuiba kutoka katika bustani ya mwingine, kuua au kumuonea mtu ambayo huelezea matendo mabaya?
Jambo hili linachanganya sana likiwekwa katika nyanja za kimataifa.
Je kufanya wema inapaswa iwe kwa ndugu na jamaa au taifa lako tuu au kwa
watu wote duniani bila kikomo.
Jambo hili ukilifikiria kwa nyanja ya kimataifa linachanganya sana
kwakua watu wa kimataifa wanauana katika vita na hawajali utu. Hata
sheria zxa sasa za kimataifa zinapata ugumu katika utekelezwaji wake.
Jambo jingine ni hadithi isemayo “Si muislam ambaye atalala akiwa kashiba huku jirani yake anakufa kwa njaa”.
Je hapa jirani alokusudiwa ni yupi?? Yani je hadithi hii ililenga
watu wa mtaani kwako, watu wa nchi yako, au ni wale waliopo ndani ya
bara lako.
Sheria hii haitakiwi iwe kwa Waislam tuu bali kwa kila mtu. Mfano mzuri ni Nchi tajiri za Ulaya na Marekani ambazo zilitawala na kufanya ukoloni barani Afrika, Ulaya na Asia.
Je walifanya kuhusiana na hadithi hii?.
Ni vigumu kuıyaepuka maswali kama haya. Hata hivyo bado utakuta
mifano mingi katika dini ya Uislam au dini nyingine ya watu waliojaribu
kujituma na kufanya matendo mazuri.
Home
News
Zaidi ya Waislam bilioni 1.5 duniani ambao waliitekeleza ibada ya ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, wamesaliwa na masaa machache ili kukamilisha ibada hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment