Watu 4 wafariki, 5 hawajulika walipo kufuatia mvua kali zilizopelekea mafuriko katika jimbo la Kentucky.
Mamlaka ya nchini Marekani imetaarifu kuwa watu wanne wamefariki na wengine watano hawajulikani walipo kufuatia mvua kali zilizopelekea mafuriko katika jimbo la Kentucky.
Timu ya uokoaji inafanya jitihada za kuwatafuta watu watano waliochukuliwa na mafuriko katika eneo la Kentucky iliyopo kusini mashariki nchini Marekani.
Utafutaji unaendelea katika eneo la milima ya Appalach ambapo mvua kali na mafuriko yanaendelea kunyesha kwa nguvu na mfululizo.
Watu 3 wametaarifiwa kupoteza maisha kufuatia mafuriko hayo, mwanaume mwenye umri wa miaka 56,mwanamke mwenye umri wa miaka 74 na mwanaume wa makamo mwenye umri wa miaka 67 wakati kituo cha habari cha NBC kimeripoti mwili wa mwanaume mwenye umri wa miaka 22 siku ya Jumatano.
Gavana wa Kentucky Steve Beshear, amefahamisha hali ya hatari katika jimbo hilo na kutoa amri ya kuongeza jitihada za kuwatafuta waliopotea.
0 comments:
Post a Comment