Image
Image

CASTRO amnyooshea kidole OBAMA kuondoa vikwazo ilivyowekewa Cuba.


Rais wa Cuba,  Bwana RAUL CASTRO  amemtaka mwenzake wa Marekani, BARACK OBAMA, kuondoa vikwazo ilivyowekewa Cuba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Amesema ana matumaini kuwa Rais OBAMA ataendelea kutumia uwezo wake kuondoa vikwazo hivyo,  ambavyo vimesababisha maisha magumu kwa wananchi wa Cuba.

Rais RAUL CASTRO  ameelezea  kupigwa marufuku  masuala ya biashara, kuwa ni kikwazo kikubwa cha kurejesha uhusiano baina ya mataif hayo mawili.

Kauli hiyo ya  Rais RAUL CASTRO imekuja,  kabla ya nchi hizo mbili hazijarejesha  uhusiano wa Kibalozi  na kufungua ofisi za balozi zao  kwenye miji mikuu ya nchi hizo Jumatatu  ijayo.

Mapema Desemba mwaka jana, Rais OBAMA alitangaza kuwa nchi yake ingeanza mazungumzo na Cuba yenye  lengo la kurejesha uhusiano wa kibalozi kwa nchi hizo mbili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment