Yeni shafak: Waziri mkuu asema Uturuki imeonyesha nguvu zake
Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema kuwa Uturuki imedhihirisha nguvu zake katika makabiliano na makundi ya kigaidi. Davutoglu alisema haya katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Istanbul. Davutoglu alisema kuwa lengo la mashambulizi yanayotekelezwa na jeshi la Uturuki ni kulinda Uhuru na demokrasia, kuendeleza utulivu katika jamii na kudhihirisha kwa wale wanaojaribu kushambulia Uturuki kuwa Uturuki ni nchi yenye nguvu
Milliyet: Shirika la teknilojia la Uturuki latazamia soko ya dunia.
Shirika la teknolojia la Etiya lililoanzishwa na Aslan Dogan linatazamia kupanuka na kuwa shirika la kimataifa. Shirika hilo limeanza kupokea miradi kutoka nchi ya Kanada na nchi za Kiarabu. Akiongea kuhusu ufanisi wa shirika lao, Dogan alisema kuwa sasa wanatazamia soko ya Ulaya na Asia.
Star: Shindano la kuogelea kutoka bara asia hadi Ulaya
Mashindano ya kuogelea ya Istanbul yaliandaliwa kwa mara ya 27 mwaka huu huku waogeleaji 1870 kutoka nchi 49 wakishiriki. Bertug Choskun alitwaa ushindi katika kitengo cha wanaume huku Nilay Erkal akitwaa ushindi katika kitengo cha wanawake.
Hurriyet: Mwanamuziki Inna aandaa video ya wimbo wake mjini Istanbul
Mwanamuziki maarufu Inna ambaye alipata unaarufu mkubwa kutokana na Albamu yake kwa jina "Hot" katika mwaka wa 2008 anaandaa video ya wimbo wake kwa jina "Party never ends" katika soko maarufu la Kapalicharshi. Kapalicharshi inatambulika kama moja ya masoko maarufu zaidi duniani.
0 comments:
Post a Comment