Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Busamba katika
halmashauri hiyo ya musoma vijijini
mkoani mara,amesema baada ya kupata taarifa kuhusu wavuvi hao kuvua samaki kwa kutumia sumu,walipiga yowe na
kwamba kabla ya wananchi wa kitongoji
hicho cha egenge kukusanyika katika eneo hilo,wavuvi hao walikimbia na
kutelekeza samaki na nyavu zilizohusika kwa kuvulia samaki hao.
Kwa upande wake diwani wa kata ya etaro anayemaliza
muda wake Bw. Paul Salamba,amesema uvuvi huo umekithiri katika eneo hilo na
kwamba licha ya kujulisha mamlaka husika
lakini hadi sasa hakuna hatua ambazo zimechukuliwa, hatua ambayo pia imekuwa ikitafasiliwa
inawezekana kuna baadhi ya maafisa wa
idara ya uvuvi ambao wamekuwa wakijihusisha na uvuvi huo haramu.
Hata hivyo samaki hao na nyavu zilizohusika katika
uvuvi huo haramu zimetekezwa kwa mto
chini ya ulinzi wa wananchi wenyewe pamoja na askari wa jeshi la Polisi katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment