Katibu wa chama cha CHP alaani vikali shambulio la Sanliurfa.
Baada ya kulipuka kwa bomu na kusababisha vifo vya watu 31 na kuwajeruhi wengine katika bustani inayopatikana katika jumba la utamaduni la meya wa Suruc, katibu wa chama cha CHP Kemal Kilicdaroglu amelaani vikali shambulio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika mkoa wa Sanliurfa, mkoa ambao unapatikana kusini –kaskazini mwa Uturuki.
Kilicdaroglu alifahamisha katika akaunti yake ya Twitter tukio hilo lime limeiacha Uturuki katika majonzi na uzuni na kusema kuwa analaani vikali ugaidi na wote wale wanaochochea ugaidi.
0 comments:
Post a Comment