Mchungaji mmoja wa kanisa mwenye umri wa miaka 24 alikamatwa na Polisi mwishoni mwa Juma Afrika Kusini akituhumiwa kuwalisha nyoka hai waumini wake kanisani.
Mchungaji huyo mwenye msimamo mkali aliwambia waumini wake kuwa nyoka hizo zina ladha ya chokoleti yule ambae atakula akiwa na imani thabiti.
Mchungaji huyo ambae anatambulika kwa jina la Penuel Mnguni alikamatwa baada ya kuonekana kwa picha katika mtandao wa kijamii wa Facebook akiendesha tukio hilo.
Kiongozi katika shirika la kutunza wanyama Afrika SPCA limemshataki mchungaji huyo kwa kusema kuwa nyoka hailiwi ikiwa nzima na kuzidi kufahamisha kuwa kitendo hicho kimewaathiri watoto walikuwa katika kanisa hilo.
Shirika la SPCA linamshtumu pia Mchungaji huyo kuwalisha "kondoo" wake panya na mijusi.
Mwaka 2014, mchungaji mwingine aliwalisha waumni wake majani.
Taarifa zinafahamisha kuwa mchungaji Penuel ni mmoja miongoni mwa wafuasi wa Mchungaji huyo.
0 comments:
Post a Comment