Image
Image

Israel yaidhinisha hukumu ya kifungo cha miaka 20 gerezani kwa Wapalestina wanaorusha mawe.


Bunge la Israel limepitisha muswada unaopendekeza hukumu ya kifungo cha miaka 20 gerezani kwa Wapalestina wanaorusha mawe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti la Yediot Ahranot nchini Israel, muswada huo uliopitishwa bungeni utaiwezesha Israel kutoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 gerezani kwa Wapalestina wanaorusha mawe kwa lengo la kusababisha hasara.
Vile vile Wapalestina wanaobeba mawe pasi na kuwa na nia ya kusababisha hasara nao wataweza kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 10 gerezani.
Mkuu wa kituo cha kutetea haki za kibinadamu Fuad el-Hafash, alisema kwamba Israel inazidi kuzua utata kutokana na baadhi ya vitendo vya ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina kwa kupitisha muswada huo.
Hafash alisema, ‘‘Wapalestina waliokuwa chini ya shinikizo la Israel wataendelea na makabiliano kwa kutumia mawe na vifaa vinginevyo. Israel nayo inajaribu kukabiliana na Wapalestina kivyovyote vile.’’
Waziri wa Sheria wa Israel Ayelet Shaked, anaarifiwa kuandaa sheria hiyo mpya ya hukumu kali kwa Wapalestina wanaokabiliwa na mashataka ya kurusha mawe.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment