5 wauawa kwenye mapigano kati ya vikosi vya UN vya kulinda amani na kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Watu wasiopungua watano wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mapigano yaliyozuka kati ya vikosi vya UN vya kulinda amani (MINUSCA) na kundi la waasi katika mji mkuu wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa MINUSCA, waasi wanne pamoja na mwanajeshi mmoja waliuawa katika mapigano hayo.
Msemaji wa eneo hilo lililozuka mapigano hayo pia alitoa maelezo na kusema kwamba kikosi cha MINUSCA kilikuwa kimevamia kwa lengo la kutaka kumkata kiongozi wa kundi la waasi la Seleka, Harun Gaye.
Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikumbwa na mizozo kati ya kundi la Anti-Balaka na Seleka tangu mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment