Amesema kizazi hiki ni cha mwisho chenye kushughulikia suala hilo na kwamba imelazimu Marekani kuchukua hatua.
Obama amesisitiza hatua kali kuchukuliwa haraka, kupunguza gesi ya ukaa inayotoka katika viwanda nchini Marekani, theluthi moja, ifikiapo mwaka 2030.
Wachambuzi wa mambo wanasema mpango huo unatazamwa kama changamoto kwa nchi nyingine zikielekea kabla ya mkutano mkuu utakaofanyika jijini Paris.
Umoja wa Mataifa umepokea vyema mpango wa Marekani pia Umoja wa Ulaya huku ukipingwa vikali na wapinzani kutoka chama cha Republican.
0 comments:
Post a Comment