Tangu
kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka huu tutashuhudia mabadiliko
makubwa sana, mabadiliko haya siyo tu aina ya watu wanaoshiriki kwenye
kugombea nafasi mbalimbali, bali pia mfumo utakaotumika kwenye kampeni
hadi upigaji kura. Mwaka huu tutashuhudia matumizi ya Tehama kwa kiwango
kikubwa sana kwenye kampeni za uchaguzi na hata utangazaji na uchungaji
wa matokeo ya chaguzi.Tutegemee kupata updates za matokeo ya kura toka
kila kituo ndani ya dakika punde tuu wanapomaliza kuhesabu.
Kwa
chama chochote kinachotaka kufikia watu na hatimaye kushinda, ni ngumu
kufanikisha hilo bila kutumia Tehama. kwa maneno mengine, Tehama ndiyo
itakayoongoza uchaguzi wa mwaka huu. Tumeona mfano wa Obama mwaka 2008.
Akiongozwa na kauli mbiu yake ya pamoja tunaweza (Yes we can) na
matumizi ya mitandao, Obama aliweza kufikisha ujumbe kwa vijana wengi
kama ilivyo sasa kwa Tanzania, na hatimaye kushinda uchaguzi wa
kihistoria.
Kwa
Tanzania, tumeona jinsi gani vijana walivyo na chachu ya mabadiliko,
tumeona ni jinsi gani vijana walivyokuwa wanakesha kwenye vituo vya
kujiandikisha ili kupata kadi zao za kupigia kura. Ni vijana hawa ambao
wamelala kwenye matumizi ya Teknolojia. Wao wanalala na Instagram,
wanaamka na Twitter mchana wanashinda Whatsapp huki jioni wakitembelea
Facebook. Iwe kwa kutumia komputa mpakato (Laptop) au kwa simu za
mikononi. Haijalishi kijana huyu yupo kule kwetu Nyamwimbe au Mbezi
Beach Goig, wote wanafikiwa na taarifa kwa uharaka wake.
Mitandao ya kijamii, kama Facebook,
Twitter, Whatsapp, Instagram nk itachukua nafasi ya kipekee kabisa
mwaka huu. Nakumbuka, Uchaguzi wa mwaka 2010 mitandao kama Jamii Forums
ilijizolea umaarufu sana, ila mwaka huu tutegemee mambo tofauti sana.
Hebu tuangalie sababu zitakazosukuma matumizi ya Tehama kwa mazingira ya Tanzania.
Tabia za Watanzania.
Moja
ya sifa kuu ya Watanzania, ni kutopenda kusoma makala ndefu,na sifa hii
inaenda nchi nyingi Africa, ndiyo sababu kuna masihala wazungu husema,
ukitaka kumnyima kitu muafrica, weka kwenye kitabu. Wengi hupenda picha
na maelezo mache yaliyo rahisishwa (Summary). Kwenye kitabu chake
cha How to Win Campaigns, Communications for Change, Chris Rose alisema,
"Moja ya nguzo muhimu ya kushinda kampeni ni kuwajua unaowafanyia
kampeni".
Kuwajua
haimaanishi kuwajua kwa majina, la hasha, bali kitabia na kimazoea. Hii
ni kwa sababu utahitaji kuwafikishia ujumbe utakaoeleweka na wao wawe
tayari kuupokea halafu ndiyo waukubali.Na kama unataka kuwafikia
Watanzania, basi achana na makala ndefu, hawatosoma.
Mitandao
Jamii na Blogu nyingi zimejikita kwenye nadharia hii, Picha na ujumbe
mfupi, na jinsi watu wanavyotazama au kuipenda (like) makala yako,
ndivyo inavyozidi kuonekana. Kwe wengi wetu, hiki si kipindi tena cha
kuongea logic, ni kipindi cha emmotion hivyo wagombea wanatakiwa kucheza
na emottion za watu zenye kujenga.
Uwingi wa Muda
Ukweli
usiopingika ni kuwa, wengi wa Watanzania wana muda mwingi wa kujadili
mambo mbalimbali,(wengi hawana kazi, hasa vijana) hii inapelekea wengi
wao kutokuwa busy kwenye shughuli wanazozifanya. Hivyo muda mwingi
wamekuwa online wakitafuta habari, na kama vijana wanavyosema, uchaguzi
ndiyo habari ya mujini.Na wao wameshaipata.
Hivyo,
kama wewe ni mmoja wa wagombea basi utahitaji kujikita sana kushibisha
njaa hii ya habari wanaoitafuta kwa aina tofautitofauti.
Uwezo wa kupambanua
Kwenye
ulimwengu wa Tehama, kuna lundo la taarifa, taarifa hizi zipo za
kujenga na kubomoa. Leo hii tumeshuhudia kwenye mitandao ya Whatsapp
taarifa jinsi zinavyozunguka tena kwa kasi ya ajabu. Na nyingi ya
taarifa hizi si za kweli au hazijengi. Leo hii mtu anaweza kuamua
kutunga taarifa na ndani ya dakika tano imeshasambaa nchi nzima bila
kujali uhalali au umuhimu wake.
Wengi
wetu tumekuwa tukisambaza bila hata kumaliza kusoma au kutafakari.
Hivyo, kwenye kipindi hiki cha ushaguzi tutegemee sana mafuriko ya
habari zisizo na tija.
Nimewahi
kuongea na Kada mmoja wa chama fulani, akaniambia, Chama chetu kina wio
mpana hadi vijijini sehemu ambazo wengi wa washindani wetu hawawezi
kufika. Sikuongea mengi, nilimuambia kitu kimoja tu, ila Teknolojia
imefika, hata kwa uchache wake. Na watu wa huko, wengi hawana hata huo
muda wa kupoteza kupambanua, wao huamini wanachokipokea. Na moja ya
nyenzo kuu kwenye kampeni ni kuwa midomoni au akilini mwa watu.Wengi
hupiga kura kwa mkumbo.
Tumeshaanza
kuona matumizi makubwa ya Teknolojia,lakini, kampeni ni kama biashara,
lazima uwe na uwezo wa kupima maendeleo na faida ya uwekezaji (ROI) ili
kuepuka kuja kushangazwa siku ya mwisho. Kuna njia bora na thabiti za
kutumia na kuongoza Teknolojia ili ije kuwa na manufaa makubwa kwenye
kampeni yako. Tukutane kwenye makala ya pili nitakapoongelea matumizi
bora ya Teknolojia kwenye Kampeni.
Makala zaidi za IT Kibiashara, tembelea https://www.dudumizi. com/blog.html
Mkata Nyoni (MSc, IT Economics, ITIL)
Founder: Dudumizi Technologies
0 comments:
Post a Comment