Image
Image

Azam FC bingwa Kagame,yaichapa Gor Mahia 2-0 na kuweka rekodi ya kihistoria.

KLABU ya Azam FC imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Kagame huku ikiweka rekodi kibao,baada ya kuitandika Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).
Rekodi ya kwanza ya Azam katika michuano hiyo ni kuwa timu ya kwanza ya Tanzania mbali na Simba na Yanga SC kutwaa taji hilo, huku ikiwa ni mara yao ya tatu kushirikishi mashindano hayo.
Rekodi ya pili ya Azam ni kutwaa kombe hilo kwa mara yao ya kwanza, huku ikiwa ni fainali yao ya pili kucheza, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2012, dhidi ya Yanga, walipoteza kwa mabao 2-0.
Rekodi ya tatu ya Azam ni kumaliza michuano hiyo bila ya kuruhusu bao lolote wavuni kwake ndani ya dakika 90 za mchezo, huku ikiifanikiwa kutwaa ubingwa huo kila kupoteza mchezo hata mmoja.
Azam imeshinda mechi zake zote kuanzia Kundi C, mbali na mchezo wa leo, nusu fainali walikutana na KCCA na kushinda 1-0, katika robo fainali walikutana na Yanga na kushindwa kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 dakika 90, hatua ya makundi walishinda.
Kwa ushindi huo, Azam inazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 30,000 (Sh. Milioni 60), wakati Gor Mahia wanapozwa na dola 20,000 (Sh. Miliioni 40).
Bao la kwanza la Azam lilifungwa dakika ya 16, kupitia kwa nahodha wake, John Bocco ‘Adebayor’ aliyemalizia krosi ya Kipre Tchetche.
Kipre Tchetche aliimaliza Gor Mahia kwa Kuifungia Azam bao la pili dakika ya 64 kwa shuti la mpira wa adhabu lililokwenda moja kwa moja langoni kwa Gor Mahia na kumshinda kipa wake Boniphace Olouch.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment