Jimmy Winfrey meneja wa zamani wa rapper Young Thug, na mshitakiwa namba
moja anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia Lil Wayne na msafara wake mwezi
April, amesema Bosi wa Cash Money Birdman nae alihusika katika upangaji wa
tukio hilo.
Mtandao wa TMZ ambao umedai kuona nyaraka za maelezo aliyoyatoa Jimmy,
yakieleza kuwa mlengwa mwingine wa mashambulizi hayo alikuwa ni muhasibu wa
kampuni ya Cash money.
Taarifa na ‘data’ za simu zinaonesha kwamba, masaa mawili kabla ya shambulio
kutokea mshitakiwa aliwasiliana na namba inayoaminika kuwa ni ya Rapper
Birdman.
Birdman na mwanae Lil wayne, wametajwa kuwa kwenye ‘battle’ nzito ya
kudaiana dolla za kimarekani $51 million.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment