Rais MUHAMMADU BUHARI wa Nigeria ametoa muda wa miezi mitatu kwa wakuu wapya wa jeshi la
nchi hiyo kuhakikisha wanakishinda kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram.
Alitoa agizo hilo wakati wa sherehe ya kuwaapisha wakuu wapya wa jeshi aliowateua mwezi
uliopita kutimiza ahadi yake baada ya kushika madaraka kwamba atakiangamiza kikundi
hicho.
Katika mkakati huo Bwana BUHARI amekikuza kikosi cha kanda chenye wanajeshi 8,700 kutoka
Nigeria na nchi jirani za Cameroon, Niger, Chad na Benin ili kukabilioana na wapiganaji
wa Boko Haram.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu Amnesty International
watu wapatao 17,000 wameuawa tangu kikundi hicho kianze maasi yake miaka 2009.
Home
Kimataifa
BUHARI atoa miezi mitatu kwa wakuu wapya wa jeshi la nchi hiyo kukikabili kikundi cha BOKO HARAM.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment