WACHEZAJI watatu wa Klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Oscar
Joshua na Amis Tambwe, wapo hatihati kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii
dhidi ya Azam utakaopigwa Jumomosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kutokana na kuugua malaria.
Mkuu wa kitengo cha Habari wa klabu
hiyo, Jerry Muro, alisema wachezaji hao wote wanasumbuliwa na malaria
lakini bado wapo kambini.
Alisema kikosi chao kilichotarajiwa kurejea Dar es Salaam jana,
kikitokea mkoani Mbeya, wanaendelea kuwepo kambini kwa kuwa wanaweza
kupata nafuu na kucheza mchezo huo.
Muro alisema wachezaji hao wanaendelea na matibabu na ana amini hadi Jumamosi na anaweza wakawa wamepona.
Alisema wanatambua umuhimu wa mchezo huo ndio maana nyota hao bado wameendelea kuwepo kikosini.
Muro alisema wamerejea kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya Dar es
Salaam , ambayo nitofauti na ile ya Mbeya, ambayo imechangia kwa
wachezaji wao hao kuumwa.
Alisema katika kambi yao, wameweza kushinda mechi zote na kikosi chao
kuzidi kuimarika kabla ya mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya.
Pia Muro alisema klabu yao imeamua kumsajili mchezaji Vicent Bosou, baada ya kuridhishwa na uwezo wake.
Muro alisema mchezaji huyo kutoka nchini Togo, amepewa mkataba wa miaka miwili kuitimikia klabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment