WANAWAKE wajawazito wapatao 150 wananufaika na huduma ya uzazi bora
katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ wilayani Kilwa mkoani Lindi, kutokana
na kijiji hicho kupata mapato ya uvunaji wa misitu ambayo yanakua kila
mwaka hadi kufikia milioni 90 kwenye akaunti ya kijiji hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Kijiji ya Misitu,
Maimuna Hemed, alisema kutokana na kijiji kukusanya mapato yanayokuwa
kutokana na utunzaji na uvunaji wa misitu, kijiji kimejipanga kuboresha
huduma za kijamii ikiwemo kumkinga mama ili aweze kupata uzazi salama.
Alisema kuwa huduma hizo zinatokana na mapato hayo ni zimekuwa na
matokeo makubwa kwa jamii hivyo kuipa nafasi jamii yao kunufaika kwa
upande wa kuwasaidia wamama wajawazito ili waweze kununulia vifaa vya
kujifungulia ili kupungua vifo vya mama na watoto.
Hemed alisema kuwa wanawake wengi walikuwa wakishindwa kugharamia
vifaa vya kujifungulia hali ambayo ilikuwa ikichangia wanawake wengi
kujifungulia nyumbani hivyo kuhatarisha maisha yao.
Alisema kuwa ili kunusuru maisha ya mama na mtoto, Kamati ya Kijjiji
ya Misitu ilikaa na kukubaliana mapato hayo yatolewe kwa wanawake
wajawazito wanaokaribia kujifungua.
Hata hivyo, aliongeza kuwa pamoja na changamoto ya kutokuwepo kwa
zahanati ya uhakika, lakini wanajitahidi kutumia mapato hayo ili
kusaidia huduma ya uzazi ambayo kwa muda mrefu imekuwa na ikihitajika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment