MKONGWE wa filamu za kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amewatolea uvivu
wasanii wenzake ambao wanakubali kutumika kisiasa katika kipindi cha
kampeni za uchaguzi bila kujua madhara watakayopata baada ya uchaguzi.
Nora alisema anawashangaa baadhi ya
wasanii kukubali kununulika wakati wakijua kuwa baada ya uchaguzi
watamwagwa na hakuna jambo la maana ambalo watafanyiwa baada ya uchaguzi
kumalizika.
Alisema thamani ya wasanii haipo na ndio maana kila uchaguzi
wanatumiwa vibaya na kuachwa solemba na kudai kuwa kila uchaguzi
ukikaribia viongozi hujiweka karibu na wasanii na baada ya hapo
wanawabwagwa.
“Nawashangaa wasanii wanaojipendekeza kwa viongozi msimu huu wa
uchaguzi alafu wao wenyewe baadaye wakiachwa wanaanza kulalamika kikubwa
wanatakiwa kujipima wao kwanza kabla hawajaingia katika siasa,”
alisema.
Nora alisema kwa upande wake hayupo tayari kutumika kisiasa alaafu
baadaye akaachwa solemba ni bora akaendelea kufanya mambo yake ya msingi
kuliko kutumika na baadaye kumwagwa.
Alisema wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu matatizo wanayokumbana
nayo lakini hakuna kiongozi yoyote kwenye siasa amewahi kujitokeza na
kuwatatulia matatizo yao lakini kipindi hiki cha uchaguzi ndio wanawaona
wa maana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment