Hali hiyo ilijitokeza jana, kufuatia kauli Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kudai kuwa uongozi wa CCM umepata taarifa kuwa UKAWA wanatengeneza kadi feki na kuzisambaza kwa wananchi huku wakifanya maigizo ya kuzirejesha na kudai wamehama CCM.Nape amesema kuna mchezo mchafu ambao unafanywa na Ukawa wa kutengeneza kadi feki na kuzigawa kwa makundi ya watu ili inapofikia kipindi cha kampeini watu hao wajitokeze kwa UKAWA na kujidai wamehama CCM.
Katika hali hiyo ya kujihami, Nape aliwatishia wananchi kwa madai kwamba yoyote ambaye atabainika kuhama CCM kwa kutumia kadi hizo feki hatachukuliwa hatua kali pamoja na wahusika kutoka UKAWA.
Akizungumzia malalamiko yaliyojitokeza kwenye chaguzi mbalimbali za kura za maoni kuwa yanahusiana na vitendo vya rushwa, amesema malalamiko hayo hayahusiani na rushwa bali ni kutokana na kukiukwa kwa taratibu na kanuni za uchaguzi.
Nape ambaye naye ni kati ya wagombea ambao walituhumiwa kwa rushwa, amesema chama hicho kina wala rushwa ambao wanasababisha kuwepo kwa malalamiko.
Mbali na hilo aliwataka wagombea wote ambao hawakuridhika na matokeo wafuate taratibu za kupeleka malalamiko yao katika ngazi ya juu ya uongozi ambayo ilikuwa hukihusika katika usimamizi pamoja na nakala kwa katibu mkuu.
“Hatuwezi kushughulikia matatizo ambayo yanatolewa katika vyombo vya habari wala malalamiko ya barabarani, tutatenda haki hata kwa kutengua matokeo pale tu ambapo tutahakikisha kuwa mlalamikaji kaonewa kweli.
“Utaratibu wa Chama chetu unafahamika siku zote mtu ambaye anaona hajatendewa haki anatakiwa kipeleka malalamiko yake katika ngazi ambazo zinastahili hivyo kila mmoja aelezwe hivyo,” amesema Nape.
Sambamba na hilo alisema vikao ndani ya CCM kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali vimeanza leo, Agosti 8 hadi 9 ni Sekretalieti, 10 hado 11 vikao vya Kamati Kuu na 12 hadi 13 ni vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM.
Hata hivyo kwa sasa kuna malalamiko mengi kwa wagombea walioshindwa katika kura za maoni kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya rushwa.
Mbali na hilo waliowengi wametangaza kuondoka CCM na kujiunga katika vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani.
0 comments:
Post a Comment