China imewaadhibu watu 197 kwa madai ya kueneza mitandaoni habari za uongo kuhusu kuanguka kwa soko la hisa nchini humo na milipuko mibaya katika mji wa Tianjin ambapo watu 150.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China la Xinhua miongoni mwa watu waliokamatwa ni mwandishi mmoja wa habari na maafisa wa soko la hisa lakini shirika hilo la habari la China halikutoa maelezo zaidi.
Hisa za China zilianguka kwa karibu asilimia nane baada ya wiki ya biashara tete iliyoeneza hofu kwa masoko mengine ya hisa duniani na hivyo kutishia uchumi wa dunia.
Kwa upande wa milipuko ya maghala yanayosadikiwa kuwa ya kemikali kwenye bandari Tianjin mbali na watu 150 waliokufa wengine 23 bado hawajaonekana huku wengine 367 wakiwa bado wamelazwa hospitalini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment